Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 47 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ ءَامِنُواْ بِمَا نَزَّلۡنَا مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبۡلِ أَن نَّطۡمِسَ وُجُوهٗا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰٓ أَدۡبَارِهَآ أَوۡ نَلۡعَنَهُمۡ كَمَا لَعَنَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلسَّبۡتِۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ مَفۡعُولًا ﴾
[النِّسَاء: 47]
﴿ياأيها الذين أوتوا الكتاب آمنوا بما نـزلنا مصدقا لما معكم من قبل﴾ [النِّسَاء: 47]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi watu wa Kitabu , Aminini na mufuate kivitendo yale tuliyoyateremsha kwenye Qur’ani, yenye kusadikisha Vitabu vilivyoko kwenu, kabla hatujawaadhibu kwa matendo yenu mabaya tukazifuta nyuso na kuzigeuza upande wa migongo au tukawapa laana waharibifu hawa kwa kuwageuza kuwa manyani na nguruwe, kama tulivyowapa laana watu wa Jumamosi ambao walikatazwa kuvua siku hii wasikatazike, Mwenyezi Mungu Akawakasirikia na Akawafukuza kutoka kwenye rehema Yake. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kupita kwa hali yoyote |