Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 56 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا سَوۡفَ نُصۡلِيهِمۡ نَارٗا كُلَّمَا نَضِجَتۡ جُلُودُهُم بَدَّلۡنَٰهُمۡ جُلُودًا غَيۡرَهَا لِيَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمٗا ﴾
[النِّسَاء: 56]
﴿إن الذين كفروا بآياتنا سوف نصليهم نارا كلما نضجت جلودهم بدلناهم جلودا﴾ [النِّسَاء: 56]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wale waliokanusha aya za Mwenyezi Mungu alizoziteremsha, wahyi wa kitabu Chake, dalili na hoja Zake, tutawaingiza kwenye Moto ambao watalionja joto lake; kila zikiungua ngozi zao tunawageuzia ngozi nyengine, ili adhabu yao na uchungu vipate kuendelea. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ni Mshindi, hakuna chochote chenye kumlemea, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake na uamuzi Wake |