Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 72 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَإِنَّ مِنكُمۡ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنۡ أَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةٞ قَالَ قَدۡ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيَّ إِذۡ لَمۡ أَكُن مَّعَهُمۡ شَهِيدٗا ﴾
[النِّسَاء: 72]
﴿وإن منكم لمن ليبطئن فإن أصابتكم مصيبة قال قد أنعم الله علي﴾ [النِّسَاء: 72]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika miongoni mwenu kuna watu wenye kujichelewesha kutoka kuenda kupambana na maadui kwa kuona uzito kufanya hivyo, na kufanya bidii kuwavunja moyo wengine kwa kusudi. Itokeapo mkapatikana kuuawa na kushindwa, huwa wakisema kwa furaha, «Mwenyezi Mungu Ametulinda kwa kutokuwako na wale waliopatikana na mambo ambayo nafsi zetu zinayachukia.» Na hilo la kutokuwa na nyinyi huwa likiwafurahisha |