Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 80 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿مَّن يُطِعِ ٱلرَّسُولَ فَقَدۡ أَطَاعَ ٱللَّهَۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ حَفِيظٗا ﴾
[النِّسَاء: 80]
﴿من يطع الرسول فقد أطاع الله ومن تولى فما أرسلناك عليهم حفيظا﴾ [النِّسَاء: 80]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yoyote mwenye kumkubali Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na akafuata uongofu wake kivitendo, basi amemkubali Mwenyezi mungu Aliyetukuka na amefuata amri Yake. Na yoyote aliyekataa kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi hatukukutumiliza, ewe Mtume, kwa hawa wenye kukataa uwe ni mtunzi wa kuyadhibiti matendo yao na kuwahesabu kwa hayo. Hesabu yao ni juu yetu |