×

Na wanasema: Tunat'ii. Lakini wanapo toka kwako kundi moja miongoni mwao hupanga 4:81 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:81) ayat 81 in Swahili

4:81 Surah An-Nisa’ ayat 81 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 81 - النِّسَاء - Page - Juz 5

﴿وَيَقُولُونَ طَاعَةٞ فَإِذَا بَرَزُواْ مِنۡ عِندِكَ بَيَّتَ طَآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ غَيۡرَ ٱلَّذِي تَقُولُۖ وَٱللَّهُ يَكۡتُبُ مَا يُبَيِّتُونَۖ فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا ﴾
[النِّسَاء: 81]

Na wanasema: Tunat'ii. Lakini wanapo toka kwako kundi moja miongoni mwao hupanga njama usiku kinyume na unayo yasema. Na Mwenyezi Mungu anayaandika yote hayo wanayo yapangia njama za usiku. Basi waachilie mbali, na umtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ويقولون طاعة فإذا برزوا من عندك بيت طائفة منهم غير الذي تقول, باللغة السواحيلية

﴿ويقولون طاعة فإذا برزوا من عندك بيت طائفة منهم غير الذي تقول﴾ [النِّسَاء: 81]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na hawa wenye kukataa, wakiwa kwenye baraza ya Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, wanajidhihirisha kuwa wanamtii Mtume na kuyafuata yale aliyokuja nayo, na wakiwa mbali na yeye na wakaondoka kwenye baraza yake, linatoka kundi katika wao likapanga njama kinyume cha yale waliyoyadhihirisha ya kumtii. Na wao hawakujua kwamba Mwenyezi Mungu Anadhibiti hesabu ya yale wanayoyapanga na kwamba Yeye Atawalipa kwa hayo malipo kamili. Basi wape mgongo na usiwajali, kwani wao hawatakudhuru. Na tegemea kwa Mwenyezi Mungu, kwani yeye Peke Yake Ndiye Mwenye kukutosha kwa usimamizi na utetezi
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek