Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 90 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿إِلَّا ٱلَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٌ أَوۡ جَآءُوكُمۡ حَصِرَتۡ صُدُورُهُمۡ أَن يُقَٰتِلُوكُمۡ أَوۡ يُقَٰتِلُواْ قَوۡمَهُمۡۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَسَلَّطَهُمۡ عَلَيۡكُمۡ فَلَقَٰتَلُوكُمۡۚ فَإِنِ ٱعۡتَزَلُوكُمۡ فَلَمۡ يُقَٰتِلُوكُمۡ وَأَلۡقَوۡاْ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَمَ فَمَا جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمۡ عَلَيۡهِمۡ سَبِيلٗا ﴾
[النِّسَاء: 90]
﴿إلا الذين يصلون إلى قوم بينكم وبينهم ميثاق أو جاءوكم حصرت صدورهم﴾ [النِّسَاء: 90]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Lakini wale wanaofungamana na watu ambao baina yenu na wao pana ahadi na mapatano, msipigane nao. Pia msipigane na wale waliowajia na nyonyo zao zina dhiki, hawataki kupigana na nyinyi na pia hawataki kupigana na watu wao, wakawa hawako na nyinyi wala hawako na watu wao, basi msipigane nao. Na lau Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Alitaka, Angaliwapa nguvu juu yenu wakashirikiana na maadui zenu washirikina katika kupigana na nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Aliwaepusha nanyi kwa fadhila Zake na uwezo Wake. Basi wakiwaacha wasipigane na nyinyi na wakawafuata na kujisalimisha kwenu, hamna njia yoyote ya kupigana na wao |