Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 15 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿رَفِيعُ ٱلدَّرَجَٰتِ ذُو ٱلۡعَرۡشِ يُلۡقِي ٱلرُّوحَ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ لِيُنذِرَ يَوۡمَ ٱلتَّلَاقِ ﴾
[غَافِر: 15]
﴿رفيع الدرجات ذو العرش يلقي الروح من أمره على من يشاء من﴾ [غَافِر: 15]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Ndiye Mtukufu Aliye juu kabisa Ambaye daraja Zake zimepaa juu sana kwa namna ya kuwa Yeye, kwa daraja hizo, Ameepukana na viumbe Vyake na kimekuwa juu cheo Chake. Yeye Ndiye Mwenye 'Arsh iliyo kubwa. Na miongoni mwa rehema Zake kwa waja Wake ni kuwatumia Wajumbe kuwapelekea wahyi ambao kwa wahyi huo wanapata uhai na kuwa kwenye mwangaza wa kuwapa muelekeo katika mambo yao, ili hao Mitume (walioletewa wahyi) wawaogopeshe waja wa Mwenyezi Mungu na wawaonye Siku ya Kiyama ambayo watakutana Siku hiyo wa mwanzo na wa mwisho |