Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 16 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿يَوۡمَ هُم بَٰرِزُونَۖ لَا يَخۡفَىٰ عَلَى ٱللَّهِ مِنۡهُمۡ شَيۡءٞۚ لِّمَنِ ٱلۡمُلۡكُ ٱلۡيَوۡمَۖ لِلَّهِ ٱلۡوَٰحِدِ ٱلۡقَهَّارِ ﴾
[غَافِر: 16]
﴿يوم هم بارزون لا يخفى على الله منهم شيء لمن الملك اليوم﴾ [غَافِر: 16]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Siku ya Kiyama watajitokeza viumbe mbele ya Mola wao, hakuna chochote kuhusu wao au kuhusu matendo yao waliyoyafanya ulimwenguni kitakachofichamana kwa Mwenyezi Mungu. Hapo Atasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, «Ni wa nani ufalme na mamlaka Siku ya Leo?» Na Ajijibu Mwenyewe, «Ni vya Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake, Mwenye kutendesha nguvu Aliyevilazimisha viumbe vyote kwa uweza Wake na enzi Yake.» |