Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 20 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿وَٱللَّهُ يَقۡضِي بِٱلۡحَقِّۖ وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَقۡضُونَ بِشَيۡءٍۗ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ ﴾
[غَافِر: 20]
﴿والله يقضي بالحق والذين يدعون من دونه لا يقضون بشيء إن الله﴾ [غَافِر: 20]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi Mungu Anahukumu baina ya watu kwa uadilifu kwa kumpa kila mtu haki yake. Na wale waungu wanaoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, hawahukumu chochote kwa kutoweza kwao kufanya hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuyasikia maneno ya waja Wake, Ndiye Mwenye kuyaona matendo wanayoyafanya, na Atawalipa kwayo |