Quran with Swahili translation - Surah Ash-Shura ayat 48 - الشُّوري - Page - Juz 25
﴿فَإِنۡ أَعۡرَضُواْ فَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ حَفِيظًاۖ إِنۡ عَلَيۡكَ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُۗ وَإِنَّآ إِذَآ أَذَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِنَّا رَحۡمَةٗ فَرِحَ بِهَاۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ فَإِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ كَفُورٞ ﴾
[الشُّوري: 48]
﴿فإن أعرضوا فما أرسلناك عليهم حفيظا إن عليك إلا البلاغ وإنا إذا﴾ [الشُّوري: 48]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watakapokataa hawa washirikina, ewe Mtume, kumuamini Mwenyezi Mungu, basi hatukukutumiliza kuwa ni mtunzi wa matendo yao mapaka ukawa ni mwenye kuwahesabu kwa hayo. Lazima yako haikuwa isipokuwa ni kufikisha ujumbe. Na sisi tunapompa binadamu rehema kutoka kwetu rehema ya utajiri, ukunjufu wa mali na mengineyo, hufurahika na akapendezwa, na unapowakumba msiba wa umasikini, ugonjwa na mengineyo kwa sababu ya kile kilichotangulizwa na mikono yao cha kufanya matendo ya kumuasi Mwenyezi Mungu, hapo binadamu huwa ni mwenye kukataa sana, huwa akihesabu misiba na akisahau neema |