×

Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), 42:51 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Ash-Shura ⮕ (42:51) ayat 51 in Swahili

42:51 Surah Ash-Shura ayat 51 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Ash-Shura ayat 51 - الشُّوري - Page - Juz 25

﴿۞ وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ ٱللَّهُ إِلَّا وَحۡيًا أَوۡ مِن وَرَآيِٕ حِجَابٍ أَوۡ يُرۡسِلَ رَسُولٗا فَيُوحِيَ بِإِذۡنِهِۦ مَا يَشَآءُۚ إِنَّهُۥ عَلِيٌّ حَكِيمٞ ﴾
[الشُّوري: 51]

Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), au kwa nyuma ya pazia, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hikima

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وما كان لبشر أن يكلمه الله إلا وحيا أو من وراء حجاب, باللغة السواحيلية

﴿وما كان لبشر أن يكلمه الله إلا وحيا أو من وراء حجاب﴾ [الشُّوري: 51]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na haipasi kwa kiumbe yoyote, kati ya binadamu, Mwenyezi Mungu Aseme naye isipokuwa kwa njia ya wahyi ambao Mwenyezi Mungu Anamtumia au Aseme naye nyuma ya pazia, kama vile Alivyosema Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, na Mūsā, amani imshukie, Au Atume mjumbe, kama Anavoyomtuma Jibrili, amani imshukie, kwa yule anayetumwa kwake ampelekee wahyi wa kile Mwenyezi Mungu Anataka apelekewe, kwa idhini ya Mola wake, na sio kwa mapendeleo yake. Hakika Yake Yeye, Aliyetukuka, Yuko juu kwa dhati Yake, majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake. Amekilazimisha kila kitu, na viumbe vyote vimemdhalilikia, ni Mwingi wa hekima katika uedeshaji Wake mambo ya viumbe Vyake. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya kusema kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa namna inayonasibiana na haiba Yake na ukubwa wa mamlaka Yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek