Quran with Swahili translation - Surah Ash-Shura ayat 52 - الشُّوري - Page - Juz 25
﴿وَكَذَٰلِكَ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ رُوحٗا مِّنۡ أَمۡرِنَاۚ مَا كُنتَ تَدۡرِي مَا ٱلۡكِتَٰبُ وَلَا ٱلۡإِيمَٰنُ وَلَٰكِن جَعَلۡنَٰهُ نُورٗا نَّهۡدِي بِهِۦ مَن نَّشَآءُ مِنۡ عِبَادِنَاۚ وَإِنَّكَ لَتَهۡدِيٓ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ ﴾
[الشُّوري: 52]
﴿وكذلك أوحينا إليك روحا من أمرنا ما كنت تدري ما الكتاب ولا﴾ [الشُّوري: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kama vile tulivyowapelekea wahyi Manabii kabla yako wewe, ewe Nabii, tulikuletea wewe wahyi wa Qur’ani itokayo kwetu, hukuwa unajua kabla yake ni vitabu vipi vilivyotangulia wala nini Imani wala zipi Sheria zinazotokana na Mwenyezi Mungu? Lakini tumeifanya Qur’ani ni mwangaza kwa watu ambao kwa huo tunawaongoza waja wetu tunaowataka kwenye njia iliyolingana sawa. Na hakika wewe, ewe Mtume, unamuelekeza na kumuongoza kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwenye njia iliyolingana sawa, nayo ni Uislamu |