Quran with Swahili translation - Surah Al-Jathiyah ayat 11 - الجاثِية - Page - Juz 25
﴿هَٰذَا هُدٗىۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ لَهُمۡ عَذَابٞ مِّن رِّجۡزٍ أَلِيمٌ ﴾
[الجاثِية: 11]
﴿هذا هدى والذين كفروا بآيات ربهم لهم عذاب من رجز أليم﴾ [الجاثِية: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hii Qur’ani tuliyoiteremsha kwako, ewe Mtume, ni uongofu wenye kuondoa upotevu, ni dalili ya haki na inamuongoza kwenye njia iliyolingana sawa atakayeifuata na akaifanyia kazi. Na wale waliozikataa aya zilizomo ndani ya Qur’ani zenye kutolea dalili Ukweli na wasiziamini, watakuwa na adhabu miongoni mwa adhabu kali zaidi Siku ya Kiyama, yenye uchungu na kuumiza |