Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahqaf ayat 19 - الأحقَاف - Page - Juz 26
﴿وَلِكُلّٖ دَرَجَٰتٞ مِّمَّا عَمِلُواْۖ وَلِيُوَفِّيَهُمۡ أَعۡمَٰلَهُمۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ ﴾
[الأحقَاف: 19]
﴿ولكل درجات مما عملوا وليوفيهم أعمالهم وهم لا يظلمون﴾ [الأحقَاف: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kila kundi la watu wema na watu waovu watakuwa tabaka mbalimbali mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, kwa matendo yao waliyoyatenda duniani, kila mmoja kulingana na daraja yake, ili Mwenyezi Mungu Awatekelezee malipo ya matendo yao. Na wao hawatadhulumiwa kwa kuongezewa maovu yao wala kupunguziwa mema yao |