Quran with Swahili translation - Surah Al-Fath ayat 1 - الفَتح - Page - Juz 26
﴿إِنَّا فَتَحۡنَا لَكَ فَتۡحٗا مُّبِينٗا ﴾
[الفَتح: 1]
﴿إنا فتحنا لك فتحا مبينا﴾ [الفَتح: 1]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sisi tumekufungulia wewe, ewe Mtume, ufunguzi ulio waziwazi, ambao ndani yake Mwenyezi Mungu Ataipa nguvu Dini Yako na Atakupa ushindi juu ya maadui wako, nao ni mapatano ya Ḥudaybiyah ambayo kwayo watu walikuwa katika hali ya amani, na likapanuka duara la ulinganizi wa Dini ya Mwenyezi Mungu, na watu wakaingia kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu mapote kwa mapote. Kwa hivyo, Mwenyezi Mung Aliyaita mapatano hayo “Ufunguzi uliofunuka” yaani uliokuwa wazi wenye kujitokeza |