×

Hao ndio walio kufuru na wakakuzuieni msiingie Msikiti Mtakatifu, na wakawazuilia dhabihu 48:25 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Fath ⮕ (48:25) ayat 25 in Swahili

48:25 Surah Al-Fath ayat 25 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Fath ayat 25 - الفَتح - Page - Juz 26

﴿هُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّوكُمۡ عَنِ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ وَٱلۡهَدۡيَ مَعۡكُوفًا أَن يَبۡلُغَ مَحِلَّهُۥۚ وَلَوۡلَا رِجَالٞ مُّؤۡمِنُونَ وَنِسَآءٞ مُّؤۡمِنَٰتٞ لَّمۡ تَعۡلَمُوهُمۡ أَن تَطَـُٔوهُمۡ فَتُصِيبَكُم مِّنۡهُم مَّعَرَّةُۢ بِغَيۡرِ عِلۡمٖۖ لِّيُدۡخِلَ ٱللَّهُ فِي رَحۡمَتِهِۦ مَن يَشَآءُۚ لَوۡ تَزَيَّلُواْ لَعَذَّبۡنَا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ عَذَابًا أَلِيمًا ﴾
[الفَتح: 25]

Hao ndio walio kufuru na wakakuzuieni msiingie Msikiti Mtakatifu, na wakawazuilia dhabihu kufika mahala pao. Na lau si wanaume Waumini na wanawake Waumini msio wajua mkawasaga na mkaingia makosani kutokana nao bila ya kujua... Mwenyezi Mungu (amefanya haya) ili amuingize amtakaye katika rehema yake. Lau wangeli tengana bila ya shaka tungeli waadhibu walio kufuru kwa adhabu chungu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: هم الذين كفروا وصدوكم عن المسجد الحرام والهدي معكوفا أن يبلغ محله, باللغة السواحيلية

﴿هم الذين كفروا وصدوكم عن المسجد الحرام والهدي معكوفا أن يبلغ محله﴾ [الفَتح: 25]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Makafiri wa Kikureshi ndio waliokataa kumpwekesha Mwenyezi Mungu, wakawazuia nyinyi, Siku ya Ḥudaybiyah, kuingia Msikiti wa al-Ḥarām, wakakataza wanyama na wakawafunga wasifike mahali pa wao kuchinjwa, napo ni Ḥarām. Na lau si wanaume Waumini walio wanyonge na wanawake Waumini msiowajua, walio kati ya hawa makafiri wa Makkah, wanaoificha Imani yao kwa kuzichelea nafsi zao, msije mkawakanyaga kwa jeshi lenu mkawaua, mkapata dhambi, aibu na gharama kwa mauaji hayo bila kujua, tungaliwapa nyinyi uwezo juu yao, ili Mwenyezi Mungu Apate kumtia kwenye rehema Zake Anayemtaka kwa kumpa neema ya kuamini baada ya kukanusha. Lau hawa Waumini wa kiume na Waumini wa kike wangalitenganika na washirikina wa Makkah na wakajitoa kati yao, tungaliwaadhibu wale waliokufuru na kukanusha miongoni mwao adhabu yenye uchungu na kuumiza
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek