×

Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu 48:29 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Fath ⮕ (48:29) ayat 29 in Swahili

48:29 Surah Al-Fath ayat 29 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Fath ayat 29 - الفَتح - Page - Juz 26

﴿مُّحَمَّدٞ رَّسُولُ ٱللَّهِۚ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ أَشِدَّآءُ عَلَى ٱلۡكُفَّارِ رُحَمَآءُ بَيۡنَهُمۡۖ تَرَىٰهُمۡ رُكَّعٗا سُجَّدٗا يَبۡتَغُونَ فَضۡلٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٰنٗاۖ سِيمَاهُمۡ فِي وُجُوهِهِم مِّنۡ أَثَرِ ٱلسُّجُودِۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمۡ فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِۚ وَمَثَلُهُمۡ فِي ٱلۡإِنجِيلِ كَزَرۡعٍ أَخۡرَجَ شَطۡـَٔهُۥ فَـَٔازَرَهُۥ فَٱسۡتَغۡلَظَ فَٱسۡتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِۦ يُعۡجِبُ ٱلزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ ٱلۡكُفَّارَۗ وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِنۡهُم مَّغۡفِرَةٗ وَأَجۡرًا عَظِيمَۢا ﴾
[الفَتح: 29]

Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: محمد رسول الله والذين معه أشداء على الكفار رحماء بينهم تراهم ركعا, باللغة السواحيلية

﴿محمد رسول الله والذين معه أشداء على الكفار رحماء بينهم تراهم ركعا﴾ [الفَتح: 29]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wale walio pamoja na yeye katika dini yake, ni wakali juu ya makafiri, wanahurumiana wao kwa wao, utawaona wakirukuu na kumsujudia Mwenyezi Mungu katika Swala yao, wakimtarajia Mola wao Awatunuku fadhila Zake, Awatie Peponi na Awe radhi nao. Alama ya utiifu wao kwa Mwenyezi Mungu iko wazi kwenye nyuso zao kwa alama ya kusujudu na kuabudu. Hiii ndiyo sifa yao kwenye Taurati. Na sifa yao katika Injili ni kama sifa ya mmea wa nafaka uliotoa kijiti chake na tawi lake, kisha matawi yakawa mengi baada ya hapo, na mmea ukashikana, ukapata nguvu na ukasimama juu ya kigogo chake ukiwa na mandhari mazuri yanayowapendeza wakulima, ili kuwatia hasira kwa Waumini hawa, kwa wingi wao na uzuri wa mandhari yao, makafiri. Katika haya pana dalili ya ukafiri wa wenye kuwachukia Maswahaba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie, kwa kuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu Anamtia hasira kwa Maswahaba basi ishapatikana kwake sababu ya hasira nayo ni ukafiri. Mwenyezi Mungu Amewaahidi waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kati yao kusamehewa dhambi zao na kupewa malipo mema mengi yasiyokatika, nayo ni Pepo. (Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya ukweli unaoaminiwa usioenda kinyume. Na kila mwenye kufuata nyayo za Maswahaba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie, basi yeye anaingia kwenye hukumu yao ya kustahiki msamaha na malipo makubwa, na wao wana ubora, kutangulia mbele na ukamilifu ambao hakuna yoyote katika ummah huu atakayewafikia, radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie na Awaridhishe)
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek