Quran with Swahili translation - Surah Al-hujurat ayat 9 - الحُجُرَات - Page - Juz 26
﴿وَإِن طَآئِفَتَانِ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱقۡتَتَلُواْ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَهُمَاۖ فَإِنۢ بَغَتۡ إِحۡدَىٰهُمَا عَلَى ٱلۡأُخۡرَىٰ فَقَٰتِلُواْ ٱلَّتِي تَبۡغِي حَتَّىٰ تَفِيٓءَ إِلَىٰٓ أَمۡرِ ٱللَّهِۚ فَإِن فَآءَتۡ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَهُمَا بِٱلۡعَدۡلِ وَأَقۡسِطُوٓاْۖ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ ﴾
[الحُجُرَات: 9]
﴿وإن طائفتان من المؤمنين اقتتلوا فأصلحوا بينهما فإن بغت إحداهما على الأخرى﴾ [الحُجُرَات: 9]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mapote mawili ya Waumini yakipigana, fanyeni upatanishi, enyi Waumini, baina yao kwa kuyaita yakubali kuamuliwa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kuridhika na uamuzi wa hivyo viwili. Iwapo pote mojawapo ya yale mawili litalifanyia uadui pote lingine na litakataa kukubali mwito huo wa upatanishi, basi lipigeni vita mpaka lirudi kwenye uamuzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na likirudi fanyani upatanishi baina ya hayo mawili kwa haki, na mfanyeni uadilifu katika uamuzi wenu kwa kutotoka nje ya hukumu ya wenyezi Mungu na hukumu ya Mtume Wake katika uamuzi wenu. Hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda waadilifu katika uamuzi wao, wanaohukumu baina ya viumbe Vyake kwa haki. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya mapenzi kwa Mwenyezi Mungu kihakika, kama inavyonasibiana na utukufu Wake Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu |