Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 1 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَوۡفُواْ بِٱلۡعُقُودِۚ أُحِلَّتۡ لَكُم بَهِيمَةُ ٱلۡأَنۡعَٰمِ إِلَّا مَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ غَيۡرَ مُحِلِّي ٱلصَّيۡدِ وَأَنتُمۡ حُرُمٌۗ إِنَّ ٱللَّهَ يَحۡكُمُ مَا يُرِيدُ ﴾
[المَائدة: 1]
﴿ياأيها الذين آمنوا أوفوا بالعقود أحلت لكم بهيمة الأنعام إلا ما يتلى﴾ [المَائدة: 1]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, timizeni ahadi za Mwenyezi Mungu zilizotiliwa mkazo za kuamini Sheria za Dini na kuzifuata, na tekelezeni ahadi mlizopeana nyinyi kwa nyinyi miongoni mwa amana mlizowekeana, biashara na mengineyo kati ya yale yasiyoenda kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Na hakika Mwenyezi Mungu Amewahalalishia wanyama wa mifugo, nao ni ngamia, ng’ombe na mbuzi na kondoo, isipokuwa yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaelezea ya kuwaharamishia mfu, damu na mengineyo; na ya kuwaharamishia kuwinda mkiwa kwenye hali ya ihramu (kwa ibada ya Hija au Umra). Kwa hakika Mwenyezi Mungu Anahukumu Anachokitaka kulingana na hekima Yake na uadilifu Wake |