Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 106 - المَائدة - Page - Juz 7
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ شَهَٰدَةُ بَيۡنِكُمۡ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ حِينَ ٱلۡوَصِيَّةِ ٱثۡنَانِ ذَوَا عَدۡلٖ مِّنكُمۡ أَوۡ ءَاخَرَانِ مِنۡ غَيۡرِكُمۡ إِنۡ أَنتُمۡ ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَأَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةُ ٱلۡمَوۡتِۚ تَحۡبِسُونَهُمَا مِنۢ بَعۡدِ ٱلصَّلَوٰةِ فَيُقۡسِمَانِ بِٱللَّهِ إِنِ ٱرۡتَبۡتُمۡ لَا نَشۡتَرِي بِهِۦ ثَمَنٗا وَلَوۡ كَانَ ذَا قُرۡبَىٰ وَلَا نَكۡتُمُ شَهَٰدَةَ ٱللَّهِ إِنَّآ إِذٗا لَّمِنَ ٱلۡأٓثِمِينَ ﴾
[المَائدة: 106]
﴿ياأيها الذين آمنوا شهادة بينكم إذا حضر أحدكم الموت حين الوصية اثنان﴾ [المَائدة: 106]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, mmoja wenu akiwa karibu na kufa, basi ni juu yake awashuhudishe wasia wake waaminifu wawili miongoni mwa Waislamu, au wawili wengine miongoni mwa wasiokuwa Waislamu ikibidi hivyo, na kusiwe na Waislamu. Hao mtawashuhudisha iwapo muko safarini kwenye ardhi na mkafikiwa na kifo. Na iwapo mtautilia shaka ushahidi wao, wasimamisheni baada ya Swala, yaani, swala ya Waislamu, hasa Swala ya Alasiri, waape kwa Mwenyezi Mungu kiapo cha dhati kwamba wao hawachukui kwa ushahidi wao thamani ya kilimwengu kama badala, wala hawamfanyii mapendeleo jamaa yao na wala hawafichi kwa kiapo chao ushahidi wa Mwenyezi Mungu uliyoko kwao na kwamba wao wakilifanya hilo, basi wao watakuwa ni miongoni mwa waliofanya hatia |