Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 107 - المَائدة - Page - Juz 7
﴿فَإِنۡ عُثِرَ عَلَىٰٓ أَنَّهُمَا ٱسۡتَحَقَّآ إِثۡمٗا فَـَٔاخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَحَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَوۡلَيَٰنِ فَيُقۡسِمَانِ بِٱللَّهِ لَشَهَٰدَتُنَآ أَحَقُّ مِن شَهَٰدَتِهِمَا وَمَا ٱعۡتَدَيۡنَآ إِنَّآ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[المَائدة: 107]
﴿فإن عثر على أنهما استحقا إثما فآخران يقومان مقامهما من الذين استحق﴾ [المَائدة: 107]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wakigundua wanaohusika na maiti kuwa wale mashahidi wawili wamefanya makosa ya hiana katika ushahidi au wasia, basi na wasimame mahali pao pa ushahidi watu wawili wenye ujamaa na aliyekufa waape kwa Mwenyezi Mungu: Ushahidi wetu wa kweli unastahiki zaidi kukubaliwa kuliko ushahidi wao wa urongo. Na sisi hatukukiuka haki katika kutoa ushahidi wetu. Na tukifanya dhuluma na kutoa ushahidi usio wa haki, basi sisi tutakuwa ni miongoni mwa madhalimu wenye kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu |