×

Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao 5:13 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:13) ayat 13 in Swahili

5:13 Surah Al-Ma’idah ayat 13 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 13 - المَائدة - Page - Juz 6

﴿فَبِمَا نَقۡضِهِم مِّيثَٰقَهُمۡ لَعَنَّٰهُمۡ وَجَعَلۡنَا قُلُوبَهُمۡ قَٰسِيَةٗۖ يُحَرِّفُونَ ٱلۡكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِۦ وَنَسُواْ حَظّٗا مِّمَّا ذُكِّرُواْ بِهِۦۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَآئِنَةٖ مِّنۡهُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۖ فَٱعۡفُ عَنۡهُمۡ وَٱصۡفَحۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ﴾
[المَائدة: 13]

Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema

❮ Previous Next ❯

ترجمة: فبما نقضهم ميثاقهم لعناهم وجعلنا قلوبهم قاسية يحرفون الكلم عن مواضعه ونسوا, باللغة السواحيلية

﴿فبما نقضهم ميثاقهم لعناهم وجعلنا قلوبهم قاسية يحرفون الكلم عن مواضعه ونسوا﴾ [المَائدة: 13]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kwa sababu ya hawa Mayahudi kuvunja ahadi zao zilizotiliwa mkazo, tuliwafukuza kutoka kwenye rehama yetu na tukazijaalia nyoyo zao kuwa ngumu, hazilainiki kwa Imani, wanayageuza maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo Alimteremshia Mūsā, nayo ni Taurati, na wakaacha kuitumia sehemu ya yale waliyokumbushwa nayo. Na utaendelea , ewe Mtume, kupata kutoka kwa Mayahudi uhaini na uvunjaji ahadi, kwani wao wako kwenye njia ya mababu zao, isipokuwa wachache miongoni mwao. Basi samehe kwa mabaya wanayokutendea na usiwe na chuki juu yao. Hakika Mwenyezi Mungu Anampenda anayefanya uzuri wa kusamehe na kutokuwa na chuki kwa aliyemfanyia ubaya. (Hivi ndivyo vile watu wapotovu wanapata njia ya kufikia malengo yao mabaya kwa kuyapotoa maneno ya Mwenyezi Mungu na kuyapa maana ambayo siyo yake. Wakishindwa kupotoa na kugeuza maana, wanayaacha yale yasioafikiana na matamanio yao katika sheria ya Mwenyezi Mungu ambayo hawatathibiti juu yake isipokuwa wachache waliyohifadhiwa na Mwenyezi Mungu kati yao)
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek