Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 14 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿وَمِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّا نَصَٰرَىٰٓ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَهُمۡ فَنَسُواْ حَظّٗا مِّمَّا ذُكِّرُواْ بِهِۦ فَأَغۡرَيۡنَا بَيۡنَهُمُ ٱلۡعَدَاوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَسَوۡفَ يُنَبِّئُهُمُ ٱللَّهُ بِمَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ ﴾
[المَائدة: 14]
﴿ومن الذين قالوا إنا نصارى أخذنا ميثاقهم فنسوا حظا مما ذكروا به﴾ [المَائدة: 14]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tulichukua ahadi ya mkazo kwa wale waliodai kuwa wao ni wafuasi wa Al-Masīḥ ‘Īsā mwana wa Maryam, na hali wao sio hivyo, kama ile tulioichukua kwa Wana wa Isrāīl, kwamba watamfuata Mtume wao, watamnusuru na watamsaidia, lakini walibadilisha Dini yao na wakaacha kutumia sehemu ya yale waliyokumbushwa nayo, kama walivyofanya Mayahudi. Kwa hivyo tulitia uadui na chuki kati yao mpaka Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu Atawapa habari, Siku ya Hesabu, ya yale ambayo wao walikuwa wakiyafanya, na Atawatesa kwa matendo yao |