×

Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla 5:48 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:48) ayat 48 in Swahili

5:48 Surah Al-Ma’idah ayat 48 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 48 - المَائدة - Page - Juz 6

﴿وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَمُهَيۡمِنًا عَلَيۡهِۖ فَٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُۖ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ عَمَّا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡحَقِّۚ لِكُلّٖ جَعَلۡنَا مِنكُمۡ شِرۡعَةٗ وَمِنۡهَاجٗاۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرۡجِعُكُمۡ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ ﴾
[المَائدة: 48]

Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وأنـزلنا إليك الكتاب بالحق مصدقا لما بين يديه من الكتاب ومهيمنا عليه, باللغة السواحيلية

﴿وأنـزلنا إليك الكتاب بالحق مصدقا لما بين يديه من الكتاب ومهيمنا عليه﴾ [المَائدة: 48]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na tumekuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani. Na yote yaliyomo ndani yake ni haki, yanatoa ushahidi juu ya ukweli wa Vitabu kabla yake na kwamba -vitabu hivyo- vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, hali ya kuuthibitisha usahihi uliomo, kuufafanua upotovu uliomo na kuzifuta baadhi ya sheria zake. Kwa hivyo, wahukumu kati ya wale Mayahudi wanaoshitakiana kwako kwa sheria zile ulizoteremshiwa katika hii Qur’ani, wala usiiepuke haki, ambayo Mweyezi Mungu Amekuamrisha uitumie, ukafuata matakwa yao na yale waliyoyazoea. Kwani kila kundi la watu tumewawekea sheria na njia iliyo wazi ya wao kuifuata. N a lau Mwenyezi Mungu Angalitaka, Angalizifanya sheria zenu kuwa ni moja, lakini Yeye, Aliyetukuka, Alizifanya zitafautiane ili awape mtihani, ili mtiifu na mwenye kuasi wajulikane waziwazi. Basi yakimbilieni yale yaliyo bora kwenu katika Makao Mawili yenu(duniani na Akhera), kwa kuyafuata yaliyomo kwenye Qur’ani kivitendo. Kwani mwisho wenu ni kurudi kwa Mwenyezi Mungu; huko Atawapa habari ya yale mliyokuwa mkitafautiana juu yake, na hapo Atamlipa kila mmoja kwa amali yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek