Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 49 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿وَأَنِ ٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ وَٱحۡذَرۡهُمۡ أَن يَفۡتِنُوكَ عَنۢ بَعۡضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيۡكَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعۡضِ ذُنُوبِهِمۡۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ لَفَٰسِقُونَ ﴾
[المَائدة: 49]
﴿وأن احكم بينهم بما أنـزل الله ولا تتبع أهواءهم واحذرهم أن يفتنوك﴾ [المَائدة: 49]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hukumu, ewe Mtume , kati ya Mayahudi kwa Aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu katika Qur’ani, wala usiyafuate matakwa ya wale wanaoshitakiana kwako. Na jihadhari nao wasikuzuie na baadhi ya Aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu ukaacha kuyatumia. Na iwapo wataikataa hukumu unayoitoa, basi jua kwamba Mwenyezi Mungu Anataka kuwaepusha na njia ya uongofu kwa sababu ya madhambi waliyotangulia kuyafanya. Na kwa hakika, wengi wa watu wako nje ya utiifu wa Mola wao |