Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 68 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَسۡتُمۡ عَلَىٰ شَيۡءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُواْ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرٗا مِّنۡهُم مَّآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ طُغۡيَٰنٗا وَكُفۡرٗاۖ فَلَا تَأۡسَ عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ ﴾
[المَائدة: 68]
﴿قل ياأهل الكتاب لستم على شيء حتى تقيموا التوراة والإنجيل وما أنـزل﴾ [المَائدة: 68]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia Mayahudi na Wanaswara, «Nyinyi hamuna fungu lolote la dini, madhali hamkuyafuata kivitendo yaliyomo ndani ya Taurati na Injili na Qur’ani aliyokuja nayo Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,.» Na hakika wengi wa wale waliopewa Kitabu, haiwaongezei kuteremshiwa wewe Qur’ani isipokuwa ni ujabari na kukanusha. Kwa hivyo, wao wanakuhusudu kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amekutuma kwa ujumbe huu wa mwisho, ambao Ameeleza humo aibu zao. Basi usiwe na huzuni, ewe Mtume, juu ya kule kukukanusha kwao |