Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 75 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿مَّا ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَ إِلَّا رَسُولٞ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهِ ٱلرُّسُلُ وَأُمُّهُۥ صِدِّيقَةٞۖ كَانَا يَأۡكُلَانِ ٱلطَّعَامَۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ ثُمَّ ٱنظُرۡ أَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ ﴾
[المَائدة: 75]
﴿ما المسيح ابن مريم إلا رسول قد خلت من قبله الرسل وأمه﴾ [المَائدة: 75]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakuwa al-Masih, mwana Maryam isipokuwa ni Mtume kama wale Mitume waliomtangulia; na mamake aliamini Imani ya dhati, kiilimu na kivitendo. Na wote wawili wanahitajia chakula kama walivyo binadamu wengineo. Na anayehitaji chakula ili aishi, hawi ni mungu. Basi izingatie, ewe Mtume, hali ya hawa makafiri.Tumekufafanulia alama zinazoonyesha upweke wetu na ubatilifu wa yale wanayoyadai kuhusu Mitume wa Mwenyezi Mungu. Kisha wao, pamoja na hilo, wanapotea njia ya haki ambayo sisi tunawaongoza waifuate. Kisha hebu angalia, vipi wanaepushwa na haki baada ya ufafanuzi huu |