Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 78 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿لُعِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۢ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُۥدَ وَعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ ﴾
[المَائدة: 78]
﴿لعن الذين كفروا من بني إسرائيل على لسان داود وعيسى ابن مريم﴾ [المَائدة: 78]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anatoa habari kwamba Amewafukuza kutoka kwenye rehema Yake makafiri miongoni mwa Wana wa Isrāīl, kama ilivyoandikwa kwenye kitabu ambacho Mwenyezi Mungu Alikiteremsha kwa Dāwūd, amani imshukie, nacho ni Zaburi, na kwenye kitabu Alichokiteremsha kwa Īsā, amani imshukie, nacho ni Injili, kwa sababu ya kuasi kwao na kuyafanyia uadui kwao mambo Aliyoyatukuza Mwenyezi Mungu Aliyetukuka |