Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 77 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا تَغۡلُواْ فِي دِينِكُمۡ غَيۡرَ ٱلۡحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوٓاْ أَهۡوَآءَ قَوۡمٖ قَدۡ ضَلُّواْ مِن قَبۡلُ وَأَضَلُّواْ كَثِيرٗا وَضَلُّواْ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ ﴾
[المَائدة: 77]
﴿قل ياأهل الكتاب لا تغلوا في دينكم غير الحق ولا تتبعوا أهواء﴾ [المَائدة: 77]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia Wanaswara, «Msiikiuke haki katika yale mnayoyaamini kuhusu mambo ya al-Masih. Wala msifuate matamanio yenu kama Mayahudi walivyofuata matamanio yao katika mambo ya dini, wakaingia kwenye upotevu, wakawafanya watu wengi wamkanushe Mwenyezi Mungu na wakatoka kwenye njia nyofu, wakaifuata njia ya upotovu na upotevu |