×

Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmeharimia katika Hija. Na 5:95 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:95) ayat 95 in Swahili

5:95 Surah Al-Ma’idah ayat 95 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 95 - المَائدة - Page - Juz 7

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقۡتُلُواْ ٱلصَّيۡدَ وَأَنتُمۡ حُرُمٞۚ وَمَن قَتَلَهُۥ مِنكُم مُّتَعَمِّدٗا فَجَزَآءٞ مِّثۡلُ مَا قَتَلَ مِنَ ٱلنَّعَمِ يَحۡكُمُ بِهِۦ ذَوَا عَدۡلٖ مِّنكُمۡ هَدۡيَۢا بَٰلِغَ ٱلۡكَعۡبَةِ أَوۡ كَفَّٰرَةٞ طَعَامُ مَسَٰكِينَ أَوۡ عَدۡلُ ذَٰلِكَ صِيَامٗا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمۡرِهِۦۗ عَفَا ٱللَّهُ عَمَّا سَلَفَۚ وَمَنۡ عَادَ فَيَنتَقِمُ ٱللَّهُ مِنۡهُۚ وَٱللَّهُ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٍ ﴾
[المَائدة: 95]

Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmeharimia katika Hija. Na miongoni mwenu atakaye muuwa makusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa kuchinja kilicho sawa na alicho kiuwa, katika mifugo, kama wanavyo hukumu waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama huyo apelekwe kwenye Al Kaaba, au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili. Mwenyezi Mungu amekwisha yafuta yaliyo pita; lakini atakaye fanya tena Mwenyezi Mungu atampa adhabu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu na Mwenye kuadhibu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الذين آمنوا لا تقتلوا الصيد وأنتم حرم ومن قتله منكم متعمدا, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الذين آمنوا لا تقتلوا الصيد وأنتم حرم ومن قتله منكم متعمدا﴾ [المَائدة: 95]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, msiue viwindwa wa barani na nyinyi muko kwenye ihramu ya Hija au Umra au mkawa muko ndani ya Haram. Na yoyote mwenye kuua kiwindwa yoyote kati ya viwindwa wa barani kwa kusudi, basi malipo yake ni achinje, miongoni mwa wanyama- howa: ngamia au ng’ombe au mbuzi na kondoo, anayefanana na kiwindwa huyo, baada ya waadilifu wawili kumfanyia makadirio, na amgawe kwa masikini wa eneo la Ḥarām au anunue chakula kwa thamani ya mfano wake na awagawie masikini wa eneo la Haram, kila masikini nusu pishi au afunge, badala yake, siku moja kwa kila nusu pishi ya chakula hicho. Mwenyezi Mungu Ameyapasisha malipo haya , ili mkosa apate matokeo ya kitendo chake. Na wale ambao ilitukia kwao kufanya lolote kama hilo kabla ya kuharamishwa, basi Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ashawasamehe. Na yoyote mwenye kurudia uhalifu huo kwa kusudi, baada ya kuharamishwa, huyo amejihatarisha kupata mateso ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu katika mamlaka Yake, na miongoni mwa enzi Yake ni kuwa Yeye atamtesa anayemuasi Akitaka, hakuna chenye kumzuia kufanya hivyo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek