Quran with Swahili translation - Surah AT-Tur ayat 21 - الطُّور - Page - Juz 27
﴿وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱتَّبَعَتۡهُمۡ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَٰنٍ أَلۡحَقۡنَا بِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَمَآ أَلَتۡنَٰهُم مِّنۡ عَمَلِهِم مِّن شَيۡءٖۚ كُلُّ ٱمۡرِيِٕۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٞ ﴾
[الطُّور: 21]
﴿والذين آمنوا واتبعتهم ذريتهم بإيمان ألحقنا بهم ذريتهم وما ألتناهم من عملهم﴾ [الطُّور: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale walioamini na wakafuatwa na watoto wao katika hiyo Imani, Tutawakutanisha watoto wao nao katika daraja yao Peponi, hata kama hawakufikia matendo ya wazazi wao, ili wazazi wafurahike na watoto wao pamoja na wao katika daraja zao. Watakusanywa baina yao kwenye hali nzuri zaidi, na hatutawapunguzia chochote katika matendo yao mema. Kila mtu anafungwa na matendo yake aliyoyachuma, hatobeba dhambi za watu wengine |