Quran with Swahili translation - Surah Al-hadid ayat 13 - الحدِيد - Page - Juz 27
﴿يَوۡمَ يَقُولُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتُ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱنظُرُونَا نَقۡتَبِسۡ مِن نُّورِكُمۡ قِيلَ ٱرۡجِعُواْ وَرَآءَكُمۡ فَٱلۡتَمِسُواْ نُورٗاۖ فَضُرِبَ بَيۡنَهُم بِسُورٖ لَّهُۥ بَابُۢ بَاطِنُهُۥ فِيهِ ٱلرَّحۡمَةُ وَظَٰهِرُهُۥ مِن قِبَلِهِ ٱلۡعَذَابُ ﴾
[الحدِيد: 13]
﴿يوم يقول المنافقون والمنافقات للذين آمنوا انظرونا نقتبس من نوركم قيل ارجعوا﴾ [الحدِيد: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Siku watakaposema wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike wakiwaambia Waumini, «Tungojeeni tupate mwangaza wa nuru yenu!» Hapo Malaika wawaambie, «Rudini nyuma yenu mtafute nuru (kwa njia ya kuwafanyia shere). Hapo watenganishwe baina yao kwa kuwekwa kizuizi cha ukuta wenye mlango ambao ndani yake , upande wa Waumini, mna rehema, na nje yake, upande wa wanafiki kuna adhabu |