Quran with Swahili translation - Surah Al-hadid ayat 14 - الحدِيد - Page - Juz 27
﴿يُنَادُونَهُمۡ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ وَلَٰكِنَّكُمۡ فَتَنتُمۡ أَنفُسَكُمۡ وَتَرَبَّصۡتُمۡ وَٱرۡتَبۡتُمۡ وَغَرَّتۡكُمُ ٱلۡأَمَانِيُّ حَتَّىٰ جَآءَ أَمۡرُ ٱللَّهِ وَغَرَّكُم بِٱللَّهِ ٱلۡغَرُورُ ﴾
[الحدِيد: 14]
﴿ينادونهم ألم نكن معكم قالوا بلى ولكنكم فتنتم أنفسكم وتربصتم وارتبتم وغرتكم﴾ [الحدِيد: 14]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hapo wale wanafiki wawaite Waumini kwa kusema, «Kwani hatukuwa na nyinyi duniani tukitekeleza ibada za Dini kama nyinyi?» Na Waumini wawaambie, «Ndio, mlikuwa na sisi kidhahiri, lakini nyinyi mlijiangamiza wenyewe kwa unafiki na kufanya maasia, na mkingojea kwa hamu Nabii afe na Waumini wapatikane na mikasa, mkakufanyia shaka kule kufufuliwa baada ya kufa, na yakawadanganya nyinyi matumaini yenu ya urongo na mkasalia katika hali hiyo mpaka mauti yakawajia. Na Shetani aliwadanganya nyinyi kuhusu Mwenyezi Mungu |