×

Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka 57:16 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-hadid ⮕ (57:16) ayat 16 in Swahili

57:16 Surah Al-hadid ayat 16 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-hadid ayat 16 - الحدِيد - Page - Juz 27

﴿۞ أَلَمۡ يَأۡنِ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن تَخۡشَعَ قُلُوبُهُمۡ لِذِكۡرِ ٱللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ ٱلۡحَقِّ وَلَا يَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلُ فَطَالَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَمَدُ فَقَسَتۡ قُلُوبُهُمۡۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ ﴾
[الحدِيد: 16]

Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ألم يأن للذين آمنوا أن تخشع قلوبهم لذكر الله وما نـزل من, باللغة السواحيلية

﴿ألم يأن للذين آمنوا أن تخشع قلوبهم لذكر الله وما نـزل من﴾ [الحدِيد: 16]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Je haujafika wakati kwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakafuata uongofu Wake kulainika nyoyo zao anapotajwa Mwenyezi Mungu na kuisikia Qur’ani, na wasiwe ni wenye ugumu wa nyoyo kama walivyokuwa wale waliopewa Vitabu kabla yao, kati ya Mayahudi na Wanaswara, ambao walipitiwa na muda mrefu wakayageuza maneno ya Mwenyezi Mungu na nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi miongoni mwao wakatoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu? Katika aya hii pana kuhimiza ulainifu na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, wakati wa kuyasikia yale Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ya Kitabu na Hekima, na kujihadhari na kujifananisha na Mayahudi na Wanaswara katika ususuwavu wa nyoyo zao na kutoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek