Quran with Swahili translation - Surah Al-hadid ayat 21 - الحدِيد - Page - Juz 27
﴿سَابِقُوٓاْ إِلَىٰ مَغۡفِرَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ وَجَنَّةٍ عَرۡضُهَا كَعَرۡضِ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ أُعِدَّتۡ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۚ ذَٰلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ ﴾
[الحدِيد: 21]
﴿سابقوا إلى مغفرة من ربكم وجنة عرضها كعرض السماء والأرض أعدت للذين﴾ [الحدِيد: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Shindaneni, enyi watu, katika kukimbilia sababu za kusamehewa kwa kutubia kidhati na kujiepusha na maasia, ili mlipwe msamaha kutoka kwa Mola wenu na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, nayo imetayarishiwa wale waliompwekesha Mwenyezi mungu na wakawafuata Mitume Wake. Hizo ni nyongeza za Mwenyezi Mungun Anazompa Anayemtaka miongoni mwa viumbe Vyake. Pepo haipatikani isipokuwa kwa rehema ya mwenyezi Mungu na nyongeza Zake na matendo mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nyongeza kubwa kwa waja Wake Waumini |