×

Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, 57:20 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-hadid ⮕ (57:20) ayat 20 in Swahili

57:20 Surah Al-hadid ayat 20 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-hadid ayat 20 - الحدِيد - Page - Juz 27

﴿ٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا لَعِبٞ وَلَهۡوٞ وَزِينَةٞ وَتَفَاخُرُۢ بَيۡنَكُمۡ وَتَكَاثُرٞ فِي ٱلۡأَمۡوَٰلِ وَٱلۡأَوۡلَٰدِۖ كَمَثَلِ غَيۡثٍ أَعۡجَبَ ٱلۡكُفَّارَ نَبَاتُهُۥ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَىٰهُ مُصۡفَرّٗا ثُمَّ يَكُونُ حُطَٰمٗاۖ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٞ شَدِيدٞ وَمَغۡفِرَةٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٰنٞۚ وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا مَتَٰعُ ٱلۡغُرُورِ ﴾
[الحدِيد: 20]

Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: اعلموا أنما الحياة الدنيا لعب ولهو وزينة وتفاخر بينكم وتكاثر في الأموال, باللغة السواحيلية

﴿اعلموا أنما الحياة الدنيا لعب ولهو وزينة وتفاخر بينكم وتكاثر في الأموال﴾ [الحدِيد: 20]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Jueni, enyi watu, kwamba uhai wa kilimwengu ni mchezo na pumbao ya miili kuchezea na nyoyo kupumbaa, na pambo la nyinyi kujipamba nalo, na kuoneshana baina yenu kwa vitu vyake vya starehe, na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama ule wa mvua ambayo mimea yake iliwafurahisha wakulima, kisha ikasinyaa na kukauka, ukaiona imekuwa rangi ya manjano baada ya kuwa rangi ya kijani, kisha ikawa ni yenye kukatikakatika na kuwa mikavu na kusagikasagika. Na huko Akhera kuna adhabu kali kwa makafiri na msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi Zake kwa watu wenye kuamini. Na haukuwa uhai wa kilimwengu, kwa mwenye kuushughulikia hali ya kusahau Akhera yake, isipokuwa ni starehe yenye udanganyifu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek