Quran with Swahili translation - Surah Al-hadid ayat 27 - الحدِيد - Page - Juz 27
﴿ثُمَّ قَفَّيۡنَا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيۡنَا بِعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَ وَءَاتَيۡنَٰهُ ٱلۡإِنجِيلَۖ وَجَعَلۡنَا فِي قُلُوبِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ رَأۡفَةٗ وَرَحۡمَةٗۚ وَرَهۡبَانِيَّةً ٱبۡتَدَعُوهَا مَا كَتَبۡنَٰهَا عَلَيۡهِمۡ إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ رِضۡوَٰنِ ٱللَّهِ فَمَا رَعَوۡهَا حَقَّ رِعَايَتِهَاۖ فَـَٔاتَيۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۡهُمۡ أَجۡرَهُمۡۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ ﴾
[الحدِيد: 27]
﴿ثم قفينا على آثارهم برسلنا وقفينا بعيسى ابن مريم وآتيناه الإنجيل وجعلنا﴾ [الحدِيد: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kisha tukafuatisha, kwenye athari za Nūḥ na Ibrāhīm, Mitume wetu tiliowatumiliza kwa hoja zilizo wazi, na tukamfuatisha 'Īsā mwana wa Maryam na tukampa Injili, na tukajaalia ndani ya nyoyo za wale waliomfuata na kuwa kwenye dini yake ulaini na huruma, wakawa wanapendana wao kwa wao, na walizusha taratibu za kuabudu, kwa kupitisha kiasi katika ibada, ambazo hatukuwalazimisha nazo isipokuwa ni wao wenyewe waliojilazimisha nazo kwa lengo la kupata radhi za Mwenyezi Mungu, lakini hawakusimama nazo vile inavyotakiwa kusimama. Basi tukawapa wale walioamini miongoni mwao malipo yao kulingana na Imani yao, na wengi miongoni mwao ni wenye kutoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na ni wenye kumkanusha Nabii Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |