Quran with Swahili translation - Surah Al-Mujadilah ayat 10 - المُجَادلة - Page - Juz 28
﴿إِنَّمَا ٱلنَّجۡوَىٰ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ لِيَحۡزُنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَيۡسَ بِضَآرِّهِمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ﴾
[المُجَادلة: 10]
﴿إنما النجوى من الشيطان ليحزن الذين آمنوا وليس بضارهم شيئا إلا بإذن﴾ [المُجَادلة: 10]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika kuzungumza kwa siri maneno ya dhambi na uadui ni katika ushawishi wa Shetani. Yeye ndiye anayeyapamba na kuyahimiza ili atie masikitiko kwenye nyoyo za Waumini. Na hilo halikuwa ni lenye kuwaudhi Waumini kitu chochote isipokuwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na mapendeleo Yake. Na kwa Mwenyezi Mungu na wajitegemeze wenye kumuamini katika mambo yao yote |