Quran with Swahili translation - Surah Al-Mujadilah ayat 21 - المُجَادلة - Page - Juz 28
﴿كَتَبَ ٱللَّهُ لَأَغۡلِبَنَّ أَنَا۠ وَرُسُلِيٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٞ ﴾
[المُجَادلة: 21]
﴿كتب الله لأغلبن أنا ورسلي إن الله قوي عزيز﴾ [المُجَادلة: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ameandika Mwenyezi Mungu kwenye Ubao Uliohifadhiwa na Amepitisha kuwa ushindi ni Wake Yeye, Kitabu Chake, Mitume Wake na waja Wake Waumini. Hakika mwenyezi Mungu, kutakasika ni Kwake, ni Mwenye nguvu, hakuna kitu kinachomuelemea, ni Mwenye ushindi juu ya viumbe Vyake |