Quran with Swahili translation - Surah Al-Mujadilah ayat 6 - المُجَادلة - Page - Juz 28
﴿يَوۡمَ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوٓاْۚ أَحۡصَىٰهُ ٱللَّهُ وَنَسُوهُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ ﴾
[المُجَادلة: 6]
﴿يوم يبعثهم الله جميعا فينبئهم بما عملوا أحصاه الله ونسوه والله على﴾ [المُجَادلة: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Mtume, Siku ya Kiyama, Siku ambayo Mwenyezi Mungu Atawahuisha wafu wote na Atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho katika uwanja mmoja, Awape habari ya yale waliyoyafanya ya kheri na shari. Mwenyezi Mungu Ameyadhibiti hayo na Ameyaandika katika Ubao Uliohifadhiwa, na Amewatunzia wao katika kurasa za matendo yao na hali wao wameyasahau. Na Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila jambo, hakuna chochote kinachofichamana Kwake |