×

Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika 58:7 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Mujadilah ⮕ (58:7) ayat 7 in Swahili

58:7 Surah Al-Mujadilah ayat 7 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Mujadilah ayat 7 - المُجَادلة - Page - Juz 28

﴿أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ مَا يَكُونُ مِن نَّجۡوَىٰ ثَلَٰثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمۡ وَلَا خَمۡسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمۡ وَلَآ أَدۡنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمۡ أَيۡنَ مَا كَانُواْۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ ﴾
[المُجَادلة: 7]

Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wane wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ألم تر أن الله يعلم ما في السموات وما في الأرض ما, باللغة السواحيلية

﴿ألم تر أن الله يعلم ما في السموات وما في الأرض ما﴾ [المُجَادلة: 7]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kwani hujui kwamba Mwenyezi Mungu Yuwajua kila kitu kilicho mbinguni na ardhini? Hawanong’oni watu watatu, kati ya viumbe Vyake, maneno ya siri isipokuwa Mwenyezi Mungu ni wanne wao , wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, wala wachache kuliko idadi hiyo iliyotajwa wala wengi kuliko idadi hiyo isipokuwa Yeye Huwa Yuko pamoja nao kwa ujuzi wake, mahali popote waliopo. Hakuna chochote kinachofichamana Kwake kuhusu mambo yao. Kisha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Siku ya Kiyama, Atawapa habari ya kile walichokifanya chema au kibaya na Atawalipa kwa walichokifanya. Hakika Mwenyezi Mungu kwa kila kitu ni Mjuzi
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek