×

Kwani huwaoni wale walio katazwa kunong'onezana kisha wakayarudia yale yale waliyo katazwa, 58:8 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Mujadilah ⮕ (58:8) ayat 8 in Swahili

58:8 Surah Al-Mujadilah ayat 8 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Mujadilah ayat 8 - المُجَادلة - Page - Juz 28

﴿أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نُهُواْ عَنِ ٱلنَّجۡوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُواْ عَنۡهُ وَيَتَنَٰجَوۡنَ بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَمَعۡصِيَتِ ٱلرَّسُولِۖ وَإِذَا جَآءُوكَ حَيَّوۡكَ بِمَا لَمۡ يُحَيِّكَ بِهِ ٱللَّهُ وَيَقُولُونَ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ لَوۡلَا يُعَذِّبُنَا ٱللَّهُ بِمَا نَقُولُۚ حَسۡبُهُمۡ جَهَنَّمُ يَصۡلَوۡنَهَاۖ فَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ ﴾
[المُجَادلة: 8]

Kwani huwaoni wale walio katazwa kunong'onezana kisha wakayarudia yale yale waliyo katazwa, na wakanong'ona juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumuasi Mtume? Na wakikujia hukuamkia sivyo anavyo kuamkia Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi hatuadhibu kwa haya tuyasemayo? Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ألم تر إلى الذين نهوا عن النجوى ثم يعودون لما نهوا عنه, باللغة السواحيلية

﴿ألم تر إلى الذين نهوا عن النجوى ثم يعودون لما نهوا عنه﴾ [المُجَادلة: 8]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Je, huwaoni, ewe Mtume, Mayahudi waliokatazwa wasizungumze kwa siri maneno yanayowatia shaka Waumini, kisha wanarudi kufanya yale waliyokatazwa, na wanazungumza kwa siri maneno ya dhambi, uadui na kuenda kinyume na amri ya Mtume? Na wanapokujia hawa Mayahudi kwa jambo lolote miongoni mwa mambo, wanakuamkia kwa maamkizi ambayo siyo yale Mwenyezi Mungu Aliyoyafanya ni maamkizi yako, na wanasema, «As-sām ‘alayka» yaani, Mauti yakushukie! Na wanasema wakiambiana wao kwa wao, «Si Atuangamize Mwenyezi Mungu kwa yale tunayomuambia Muhammad, iwapo ni Mtume kikweli.» Moto wa Jahanamu utawatosha: wataungia na watalihisi joto lake, na ubaya wa marejeo ni huo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek