×

Yeye ndiye aliye watoa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu katika 59:2 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-hashr ⮕ (59:2) ayat 2 in Swahili

59:2 Surah Al-hashr ayat 2 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-hashr ayat 2 - الحَشر - Page - Juz 28

﴿هُوَ ٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ مِن دِيَٰرِهِمۡ لِأَوَّلِ ٱلۡحَشۡرِۚ مَا ظَنَنتُمۡ أَن يَخۡرُجُواْۖ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمۡ حُصُونُهُم مِّنَ ٱللَّهِ فَأَتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِنۡ حَيۡثُ لَمۡ يَحۡتَسِبُواْۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلرُّعۡبَۚ يُخۡرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيۡدِيهِمۡ وَأَيۡدِي ٱلۡمُؤۡمِنِينَ فَٱعۡتَبِرُواْ يَٰٓأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ ﴾
[الحَشر: 2]

Yeye ndiye aliye watoa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu katika nyumba zao wakati wa uhamisho wa kwanza. Hamkudhani kuwa watatoka, nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda na Mwenyezi Mungu. Lakini Mwenyezi Mungu aliwafikia kwa mahali wasipo patazamia, na akatia woga katika nyoyo zao. Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini. Basi zingatieni enyi wenye macho

❮ Previous Next ❯

ترجمة: هو الذي أخرج الذين كفروا من أهل الكتاب من ديارهم لأول الحشر, باللغة السواحيلية

﴿هو الذي أخرج الذين كفروا من أهل الكتاب من ديارهم لأول الحشر﴾ [الحَشر: 2]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Yeye, kutakasika ni Kwake, Ndiye Aliyewatoa wale walioukanusha unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, miongoni mwa watu waliopewa Kitabu, nao ni Mayahudi wa ukoo wa Banū al Nadīr, kutoka majumbani mwao ambayo wakiwa humo walikuwa ni majirani na Waislamu pambizoni mwa Madina. Huko kulikuwa ndio mwanzo wa kutolewa nje ya Bara Arabu hadi Shām. Hamkudhani, enyi Waislamu, kuwa watatoka majumbani mwao kwa unyonge huu na utwevu, kwa silaha kali waliokuwa nazo na hifadhi ya nguvu waliokuwa nayo. Na walidhani Mayahudi kuwa ngome zao zitawakinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuwa hakuna anayeziweza. Basi amri ya Mwenyezi Mungu ilizijilia kwa namna ambayo haikupita kwenye akili zao, na Mwenyezi Mungu Akawatia hofu na kicho kikubwa, wakawa wanazivunja nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini, basi zingatieni, enyi wenye busara timamu na akili nyingi kwa hayo yaliyowafika wao
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek