Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 112 - الأنعَام - Page - Juz 8
﴿وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوّٗا شَيَٰطِينَ ٱلۡإِنسِ وَٱلۡجِنِّ يُوحِي بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ زُخۡرُفَ ٱلۡقَوۡلِ غُرُورٗاۚ وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُۖ فَذَرۡهُمۡ وَمَا يَفۡتَرُونَ ﴾
[الأنعَام: 112]
﴿وكذلك جعلنا لكل نبي عدوا شياطين الإنس والجن يوحي بعضهم إلى بعض﴾ [الأنعَام: 112]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kama tulivyokujaribu wewe, ewe Mtume, kwa maadui zako miongoni mwa washirikina, tuliwajaribu Manabii wote, amani iwashukie, kwa maadui miongoni mwa waasi wa watu wao na maadui miongoni mwa waasi wa majini, wanapelekeana wenyewe kwa wenyewe maneno waliyoyapamba kwa uharibifu, ili adanganyike mwenye kuyasikia na apate kupotea njia ya Mwenyezi Mungu. Na lau Mola wako, Aliyetukuka na kuwa juu, Alitaka, angaliweka kizuizi kati yao na ule uadui, lakini huo ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi waache na kile wanachokibuni cha urongo na uzushi |