Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 115 - الأنعَام - Page - Juz 8
﴿وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدۡقٗا وَعَدۡلٗاۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَٰتِهِۦۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ﴾
[الأنعَام: 115]
﴿وتمت كلمت ربك صدقا وعدلا لا مبدل لكلماته وهو السميع العليم﴾ [الأنعَام: 115]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na limekamilika neno la Mola wako, nalo ni Qur’ani, likiwa lina ukweli wa habari na maneno, lenye uadilifu wa hukumu. Hakuna anayeweza kuyabadilisha maneno yake yaliyokamilika. Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Ndiye Mwenye kuyasikia wanayoyasema waja Wake, Ndiye mwenye kuyajua mambo yao yaliyo waziwazi na yaliyojificha |