×

Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike 6:158 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:158) ayat 158 in Swahili

6:158 Surah Al-An‘am ayat 158 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 158 - الأنعَام - Page - Juz 8

﴿هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ أَوۡ يَأۡتِيَ رَبُّكَ أَوۡ يَأۡتِيَ بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَۗ يَوۡمَ يَأۡتِي بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفۡسًا إِيمَٰنُهَا لَمۡ تَكُنۡ ءَامَنَتۡ مِن قَبۡلُ أَوۡ كَسَبَتۡ فِيٓ إِيمَٰنِهَا خَيۡرٗاۗ قُلِ ٱنتَظِرُوٓاْ إِنَّا مُنتَظِرُونَ ﴾
[الأنعَام: 158]

Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja

❮ Previous Next ❯

ترجمة: هل ينظرون إلا أن تأتيهم الملائكة أو يأتي ربك أو يأتي بعض, باللغة السواحيلية

﴿هل ينظرون إلا أن تأتيهم الملائكة أو يأتي ربك أو يأتي بعض﴾ [الأنعَام: 158]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kwani wanangojea, hawa wenye kukataa na wakazuia watu wasiifuate njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa awajie wao Malaika wa mauti na wasaidizi wake kuzichukua roho zao au aje Mola wako, ewe Mtume, kutoa uamuzi kati ya waja wake Siku ya Kiyama, au zije baadhi ya alama za Kiyama na vitambulisho vyake vinavyoashiria kuja kwake, navyo ni kuchomoza jua kutoka upande wake wa Magharibi? Basi litakapokuwa hilo hakuna nafsi yoyote itakayofaidika na Imani yake, iwapo haikuwa imeamini kabla ya hapo, wala hayatakubaliwa matendo mema mapya ya hiyo nafsi, ikiwa ilikuwa imeamini, iwapo haikuwa imeyatenda kabla ya hapo. Waambie, ewe Mtume, «Ngojeeni kuja kwake, ili mpate kumjua aliye kwenye usawa na aliye kwenye makosa, na mtenda maovu na mtenda mema. Sisi tunalingojea hilo.»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek