Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 165 - الأنعَام - Page - Juz 8
﴿وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَٰٓئِفَ ٱلۡأَرۡضِ وَرَفَعَ بَعۡضَكُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٖ دَرَجَٰتٖ لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمُۢ ﴾
[الأنعَام: 165]
﴿وهو الذي جعلكم خلائف الأرض ورفع بعضكم فوق بعض درجات ليبلوكم في﴾ [الأنعَام: 165]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyewafanya nyinyi mushike nafasi za waliowatangulia katika ardhi baada ya Mwenyezi Mungu kuwaondoa na kuwaweka nyinyi badala yao, mupate kuiamirisha baada yao kwa kumtii Mola wenu. Na amewainua daraja baadhi yenu, katika mapato na nguvu, juu ya wengine ili kuwapa mtihani katika alichowapa miongoni mwa neema Zake, apate kuwa wazi kwa watu mwenye kushukuru na asiyeshukuru. Hakika Mola wako ni Mwepesi wa adhabu kwa aliyemkanusha na kumuasi. Na Yeye ni Mwingi wa msamaha kwa aliyemuamini na akafaya matendo mema na akatubia na dhambi yenye kuangamiza, ni Mwenye huruma Kwake. Al-Ghafūr (Mwingi wa kusamehe)na Al-Raḥīm (Mwenye kurehemu) ni majina mawili matukufu katika majina ya Mwenyezi Mungu |