Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 36 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿۞ إِنَّمَا يَسۡتَجِيبُ ٱلَّذِينَ يَسۡمَعُونَۘ وَٱلۡمَوۡتَىٰ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ ثُمَّ إِلَيۡهِ يُرۡجَعُونَ ﴾
[الأنعَام: 36]
﴿إنما يستجيب الذين يسمعون والموتى يبعثهم الله ثم إليه يرجعون﴾ [الأنعَام: 36]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wale wanaokukubali wewe, ewe Mtume, kwa yale unayoyalingania ya uongofu ni wale ambao wanayasikia maneno kwa kuyakubali. Ama makafiri, wao wamo kwenye hesabu ya wafu. Kwani uhai wa kikweli unakuwa kwa Uislamu. Na wafu, Mwenyezi Mungu Atawatoa kutoka kwenye makaburi yao wakiwa hai. Kisha watarudi Kwake Siku ya Kiyama ili watimiziwe hesabu yao na malipo yao |