Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 35 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيۡكَ إِعۡرَاضُهُمۡ فَإِنِ ٱسۡتَطَعۡتَ أَن تَبۡتَغِيَ نَفَقٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ أَوۡ سُلَّمٗا فِي ٱلسَّمَآءِ فَتَأۡتِيَهُم بِـَٔايَةٖۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَمَعَهُمۡ عَلَى ٱلۡهُدَىٰۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ ﴾
[الأنعَام: 35]
﴿وإن كان كبر عليك إعراضهم فإن استطعت أن تبتغي نفقا في الأرض﴾ [الأنعَام: 35]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na iwapo umekuwa ni mzito kwako, ewe Muhammad, upinzani wa hawa washirikina na kujiepusha kwao kukubali ulinganizi wako, basi ukiweza kujifanyia mapito ndani ya ardhi, au ngazi ya kupandia mbinguni ili uwaletee alama na dalili ya usahihi wa maneno yako, zisizokuwa hizi tulizokuletea, fanya hivyo. Na lau Mwenyezi Mungu Alitaka kuwakusanya kwenye uongofu ambao nyinyi munao na kuwaongoza kwenye Imani, Angalifanya hivyo. Lakini Hakulitaka hilo, kwa hekima Anayoijua Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake. Basi, usiwe kabisa ni miongoni mwa wale wajinga ambao huzuni zao zilizidi na wakawa na majonzi mpaka hayo yakawapelekea kwenye babaiko kubwa |