Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 37 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَقَالُواْ لَوۡلَا نُزِّلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يُنَزِّلَ ءَايَةٗ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[الأنعَام: 37]
﴿وقالوا لولا نـزل عليه آية من ربه قل إن الله قادر على﴾ [الأنعَام: 37]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na washirikina walisema, kwa ujeuri na kiburi, «Kwa nini Mwenyezi Mungu Hateremshi alama iyoneshayo ukweli wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, miongoni mwa alama za kimiujiza.» Waambie, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuwateremshia miujiza, lakini wengi wao hawajui kwamba kuteremsha miujiza kunakuwa kulingana na hekima Yake, Aliyetukuka.» |